• Swahili

     Swahili

     Karibu

  •  

    Utaratibu wa wuokovu

     

     Wokovu unatoka kwa Mungu katika Yesu Kristo, anayetupenda na mapenzi yake ni kwamba watu wote waokolewe kulingana na ahadi yake

     

     Mapenzi Ya Mungu ni kwa wote

     

    Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

    Yohana 3. 16

     

    Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.

    1 Yohana 4. 10

     

    Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

    1 Yohana 4. 16

     

    Kama vile baba awahurumiyavyo watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao. Kwa maanan Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sis tu mavumbi.

    Zaburi 103. 13-14

     

    Wanadamu ni wenye dhambi na wametengenishwa na Mungu

     

    Hakuna mwenye haki hata mmoja.

    Warumi 3. 10

     

    Maaana hakuna tofauti ; kwa sababu wote wamefanya dhambi, nakupungukiwa na utukufu wa Mungu.

    Warumi 3. 23

     

    Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti ; bali karamu ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

    Warumi 6. 23

     

    Lakini Mungu aliahidi mwokozi atakaye chukuwa dhambi zetu zote. Ni Yesu-Kristo aliye kufa na kuteseka kwa sababu ya dhambi zetu na kufufuka baada ya siku tatu

      

     Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo wake.

     Yohana 10. 11

     

    Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika wwili wake juu ya msalaba, tupate kufa kuhusu dhambi, na kuishi kwa ajili ya uadilifu ; kwa majeraha yake, nyinyi mmeponywa.

     1 Petro 2. 24

     

    Maana kwa damu yake Kristo, sisi tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa ; Ndivyo ulivyo ukuu wa neema yake.

     Waefeso 1. 7

     

     Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu, aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu. Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai ; kwa kupigwa kwake sisi tume pona. Sisi sote tumepotea kama kondoo, kila mmoja wetu ameelekea njia yake. Lakini Mwenyezi Mungu alimtwika adhabu, ambayo sisi wenyewe tuliistahili.

     Isaya 53. 5-6

     

      Damu ya kristo ilimwagika ilitupate mshamaha wa dhambi zetu. Lazima tuamini na tumpokee awe mwokozi ili tuokolewe

       

    Basi tubuni mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu.

    Matendo 3. 19

      

    Yesu akamjibu : mimi ni njia, na ukweli na uhai. Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupita kwangu.

    Yohana 14. 6

     

    Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu , nami nikiwa ndani yake , huyo huzaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.

    Yohana 15. 5

     

    Anayemwamini Mwana anao uzima wa milele ; asiyemwamini Mwana hatakuwa na uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake.

    Yohana 3. 36

     

    Lakini wale waliompokeya , wale waliomwamini, aliwaapa uwezo wakuwa watoto wa Mungu.

    Yohana 1. 12

     

     Kwa hivyo, sis sote ni wenye ndhambi na tume gawanya kutoka kwa Mungu. Lakini Mungu atupenda sana hata anataka kutupatia amani . Alituma mkombozi Yesu Kristo aliye beba dhambi zetu zote ili atufanye watoto wa Mungu.

     Anakuita ili uokolewe, Uzikaze moyo tafadhali itika ?

     

    Sikiliza ! mimi nasimama mlangoni na kubisha hodi, Mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia nyumbani kwake nakula chakula pamoja naye, naye atakula pamoja nami.

    Ufunuo 3. 20

       

    Aliye na masikio, na asikie.

     Ufunuo 13. 9

    Partager via Gmail Yahoo! Blogmarks




    Suivre le flux RSS des articles de cette rubrique